Full-Width Version (true/false)


Sisi wazee tunagombaniwa, wao vijana wanashindwa – Khadija Kopa

Msanii Mkongwe wa muziki wa Taarabu Bongo, Khadija Kopa amesema kuwa muziki huo hajashuka ila wasanii wenyewe hasa wapya ndio wameshindwa.


Muimbaji huyo amesema kuwa wasanii wapya wa sasa wameshindwa kuupeleka muziki wao mbali badala yake wasanii wa zamani bado wanang’ang’aniwa.

“Muziki hajafifia, tumefifia sisi wasanii, kuna wasanii wakubwa wa zamani tayari wameshakata tamaa na ubaya sasa hivi wasanii wapya hawatokezi sababu ya mambo mengi, kwanza wenyewe hawapendi kujishughulisha,” amesema.

“Hivyo ndivyo vimefanya tuanguke na tushindwe kutoa wasanii wapya, bado tunabakia sisi wazee tunagombaniwa, wao vijana wanashindwa kutoka nje matokeo yake wamebaki kupiga muziki kwenye mabaa, kiingilio bia,’ amesisitiza.

Katika hatua nyingine amesema si kweli kuondoka kwa Mzee Yusuph katika tasnia ya muziki kumechangia taarabu kushuka kwa kueleza kuwa hilo lilikuwepo kabla hata Mzee Yusuph hajaacha muziki.

No comments

Powered by Blogger.