Full-Width Version (true/false)


Spika ataka Mawaziri wasafiri, awapa kazi wabunge

 Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kuna haja ya wabunge kuwaombea mawaziri kwenye mamlaka husika ili wapate fursa kusafiri nje ya nchi. 
KauIi hiyo ya Spika imekuja kufuatia hoja ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ambapo alisema ni muhimu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage asafiri nje ya nchi, ili kujenga uhusiano ya kidiplomasia na kutafuta masoko ya bidhaa za mbaazi, choroko na giligilani.

Spika Ndugai ambaye alikiri kukubaliana na mchango wa Zitto Kabwe amesema ni amekiri ni kweli mawaziri inabidi wasafiri na wabunge wanapaswa kuwaombea kutoka kwenye mamlaka.

Waziri wa Biashara hawezi kukaa na sisi hapa, lazima ende, tumuombee popote pale kwenye mamlaka lazima asafiri, maana bidhaa zetu tutauza Kongwa, kuna soko huko?

Waziri wa utalii lazima asafiri ‘apige mawingu’ huko na wengine huko, ndiyo ukweli jamani, sisi wabunge lazima tuwasemee,” amesisitiza Ndugai.

No comments

Powered by Blogger.