Full-Width Version (true/false)


Stand United yatupia jicho Zanzibar 

Kiwango cha juu cha beki wa Stand United, Ali Ali kufanya vema msimu huu, kimewavutia mabosi wa Stand United 'Chama la Wana' kuona ipo haja kusajili kutoka Zanzibar.
Ali Ali ni Mzanzibar ameonyesha kiwango cha juu ikiwa ni msimu wake wa kwanza Stand United, jambo hilo limewashawishi na kuona wanaweza wakawa na kikosi makini kitakachoundwa na nyota kutoka visiwani humo.
Katibu wa timu hiyo, Kenny Nyangi ameweka wazi jambo hilo kwamba, tayari wametuma mtu anayefanya kazi ya kuangalia vipaji ambavyo vitaongeza nguvu kikosi chao.
"Tunaamini  Zanzibar kuna wachezaji wenye uwezo wa juu, ingawa si maana yangu kwamba tutawasajili kutoka huko pekee hata Bara wapo tuliowaona tumeanza kufuatilia mikataba yao," anasema Nyangi.

No comments

Powered by Blogger.