Full-Width Version (true/false)


Steve Nyerere, Aunt Ezekiel kutafuta vipaji Pangani


 TIMU  ya wasanii wa Bongo Muvi ikiongozwa na msanii wa vichekesho, Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ inatarajiwa kutua Jumamosi wiki hii wilayani Pangani mkoani Tanga kwa ajili ya kutoa elimu na fursa mbalimbali za kuibua vipaji vya wasanii.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dares Salaam, Steve  amesema Jumamosi watakuwa wilayani humo wakiwaelimisha vijana juu ya kujitambua, kutumia fursa walizonazo mkoani humo,  kama kutumia vipaji walivyonavyo ili kufanikisha malengo yao  ya kimaisha.

Amesema kuwa vijana wengi huvunjika moyo kutokana na changamoto wanazozipitia bila ya kujua watazitatua vipi,  hivyo kupitia kampeni yao ya Amka Kijana wataweza kuwapa elimu mbalimbali.

Mbali na elimu hiyo pia amesema siku hiyo kutakuwa na mtanange wa soka baina ya mashabiki wa timu ya Simba na Yanga na baadaye  watatembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vilivyomo wilayani humo.

Amesema wasanii mbalimbali kama, Aunt Ezekiel, Flora Mvungi, Jaqueline Wolper, Duma, Johari, JB na wengine wengi. Tamasha hilo litakuwa la wazi na halitakuwa na kiingilio.

No comments

Powered by Blogger.