Full-Width Version (true/false)


Steve Nyerere kuandaa tukio la kuwaombea viongozi na mastaa waliofarikiMwenyekiti wa Kikundi cha Uzalendo Kwanza, Steve Nyerere ameandaa tukio maalum litakalofanyika Jumamosi hii katika viwanja vya Leades Club jijini Dar es salaam kwaajili ya kuwaombea viongozi pamoja na mastaa waliotangulia mbele ya haki.

Muigizaji huyo amesema tukio hilo litaenda sambamba na kuwafuturisha waislamu ambao watajitokeza siku hiyo.

“Tunataka kuwakumbuka ndugu zetu waliotangulia mbele ya haki, sisi tuliobaki tunatakiwa kuwaombea ndugu zetu, sisi tupo nyuma yao kwahiyo sisi kama Uzalendo Kwanza tumeona tuandae tukio la namna hiyo ambalo kila staa na viongozi wetu aliotangulia mbele ya haki tutawaombea kwa pamoja,” alisema Steve Nyerere.

Aliongeza, “Kila aliyefariki na alikuwa anafanya shughuli ya sanaa tunapaswa kumuombea, wasanii wa filamu, wasanii wa mzuiki, watayarishaji wa muziki, waandishi wa habari ambao wamekuwa akiandika habari zetu na kutoa taarifa zetu wote tutawaombea siku ya Jumamosi hii katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam,”

Mwenyekiti huyo amesema atatoa taarifa ni viongozi gani wa serikali ambao watahudhuria shughuli hiyo ya aina yake.

No comments

Powered by Blogger.