Full-Width Version (true/false)


Stoke City yateremka rasmi daraja

Klabu ya Stoke City imeteremka rasmi daraja msimu huu baada ya kukubali kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Cystal Palace katika mchezo wa ligi uliopigwa jana.

Kichapo hicho kimeiaga rasmi Stoke iliyodumu kwa takribani miaka 10 kwenye ligi hiyo tangu ipande mara ya mwisho.

Stoke imeteremka daraja ikiwa imejikusanyia jumla ya pointi 30 pekee huku ikiwa imecheza michezo 30.

Baada ya matokeo hayo, uongozi wa Stoke ulieleza masikitiko yao kupitia ukurasa wao wa Twitter kufuatia kuteremka rasmi daraja.

No comments

Powered by Blogger.