Full-Width Version (true/false)


Sumbawanga: Ajali ya bodaboda yaua baba, mama na mtoto

 

Watu watatu wa familia moja wamefariki dunia papo hapo katika ajali iliyohusisha pikipiki na basi mali ya kampuni ya Saratoga.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, George Kyando amesema tukio hilo limetokea leo, Mei 29 saa 6 mchana katika eneo la kituo cha mafuta cha Munio, mjini hapa.


Amewataja wanafamilia Marehemu hao ni wakazi wa kitongoji cha Katandala mjini hapa.


Kamanda Kyando amesema kuwa ajali hiyo ilihusisha basi la kampuni ya Saratoga lenye namba T 211 AED aina ya Scania lililokuwa likiendeshwa na Ally Fabiano (31) mkazi wa Kigoma.


“Basi hilo lilikuwa likitokea Sumbawanga mjini kuelekea mkoani Kigoma,” amesema


Kyando amesema kuwa wanafamilia hao walikuwa wamepanda pikipiki yao iliyokuwa ikiendeshwa na Senga. 


"Ilikuwa vigumu hata kuitambua miili ya wale wazazi wa mtoto paulina kwani aliharibika vibaya lakini mtoto peke yake ndio kichwa kilionekana.” amesema Kyando.

No comments

Powered by Blogger.