Taasisi inayowatoza wanawake fedha kupitia jina la Mama Samia, yapewa za uso na serikali
Serikali kupitia Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu, Jenista Muhagama imesema aihusiki na Taasisi inayowatoza
wanawake sh. elfu kumi kumi kupitia jina la Makamu wa Rais, Mama Samia
Suluhu katika mkoa wa Kigoma.
Akijibu swali la Mbunge wa viti Maalumu Mkoa wa Kigoma,Josephine Gezebuke aliyehoji,
Katika Mkoa wa Kigoma iko NGO’s ambayo imezunguka kwa muda wa wiki mbili katika wilaya zote saba ikiwatoka wanawake sh. elfu 10, 10 na kuwapigisha picha na kuwaahidi kwamba serikali itatoa mikopo kwa kupitia mfuko wa Makamu wa Rais, Mama Samia, Je? ninataka serikali inieleze mpango huo wa kutoa pesa kupitia mfuko wa Mama Samia upo?
“Shughuli zote za uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi katika nchi yetu ya
Tanzania zinasimamiwa na sera 2004 na sheria ya uwezeshaji wananchi
Kiuchumi ya mwaka 2004 ambayo inaruhusu uanzishwaji wa Taasisi
mbalimbali kisheria, Taarifa kuhusu Taasisi hiyo zilishapatikana ndani
ya serikali na ofisi ya Makamu wa Rais ilishatoa tamko la kuikana
taasisi hiyo kwamba haihusiki nayo,” amesema Waziri Jenista.
“Ninaomba nichukue nafasi hii kuuagiza uongozi wa Mkoa wa Kigoma
kuifuatilia taaisi hiyo na kuikana na kuipa maelekezo kwamba ofisi ya
Makamu wa Rais aihusiki na jambo hilo na kama wanaendesha shughuli hizo
kwa kutumia sheria taratibu nyingine wanapaswa kujieleza kwa kutumia
sheria na taratibu zingine walizozifauta lakini sio ofisi wa Makamu wa
Rais.”
Aidha Jenista amesema kuwa kama Taasisi hiyo itaendelea kuwadanganya
wananchi kutumia mgongo wa Ofisi ya Makamu wa Rais serikali haitasika
kuchukua hatua kali.
No comments