Full-Width Version (true/false)


Tahadhari kutoka mamlaka ya hali ya hewaMamlaka ya hali ya hewa iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imewatahadharisha wananchi kuwepo kwa vipindi vya upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa pamoja na mvua zinazoambatana na radi kuanzia saa 24 zijazo kutoka sasa. 
Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na mamlaka hiyo jioni ya leo (Alhamisi) na kutaja maeneo hayo kuwa ni Ziwa Tanganyika katika mikoa ya Kigoma na Katavi.

Mbali na hilo, TMA imesema  maeneo ya Ukanda wa Ziwa Victoria pamoja na maeneo ya ukanda wa Pwani ya Kaskazini na nyanda za juu kaskzini mashariki yanatarajiwa ambayo yanatarajiwa kuwa na mvua katika maeneo machache. 

Kwa taarifa kamili angalia hapa chini..


No comments

Powered by Blogger.