Full-Width Version (true/false)


Takwimu:watu 200 huambukizwa UKIMWI kila siku Tanzania,wengi wao ni vijanaMkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania - TACAIDS, Dokta Leonard Maboko amesema hali ya maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi nchini bado ni hatarishi na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari kujikinga na maambukizi hayo. 


Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Dokta Maboko amesema vijana ni kundi lililoathiriwa zaidi na maambukizi hayo ambapo amesema watu 200 hupata maambukizi mapya kwa siku nchini na kutoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kuunga juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya UKIMWI.

Kwa mujibu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kwa mujibu wa tafiti za karibuni za Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Mkoa wa Iringa umeshika nafasi ya pili baada ya Njombe, kwa Ugonjwa wa UKIMWI.

No comments

Powered by Blogger.