Full-Width Version (true/false)


Tambwe aweka rekodi ya kipekeeMshambuliaji wa Yanga Amisi Tambwe amekuwa ni miongoni mwa wachezaji kutoka nje ya Tanzania ambao wamekuwa na uwezo mkubwa wa kufunga tangu atue nchini msimu wa 2013/14, akisajiliwa katika klabu ya Simba.
Tambwe ambaye ukubwa wa jina lake nchini aliujenga akiwa Simba baada ya kufunga mabao 19, katika msimu wake wa kwanza kwenye ligi kuu ya soka Tanzania bara, amejikuta akiweka rekodi ya kumaliza msimu huu bila kufunga hata bao moja.


Nyota huyo raia wa Burundi, alijiunga na Yanga msimu wa 2014/15 ambapo alifunga mabao 14 na kuisaidia Yanga kutwaa ubingwa wa VPL, huku katika msimu wake wa pili 2015/16 akifunga mabao 21 na kuipa Yanga ubingwa wa VPL na Kombe la FA.

Katika msimu wake wa tatu ndani ya Yanga ambao ni 2016/17 Tambwe alifunga mabao 11 ambayo pia yaliisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa VPL. Pia Tambwe alipata majeraha ambayo yameendelea hadi msimu huu.

Pamoja na kuanza msimu akiwa majeruhi, Tambwe alirejea dimbani katika mechi kadhaa lakini hakufanikiwa kufunga hivyo kumfanya amalize msimu akiwa Tanzania bila kufunga kwa mara ya kwanza.

No comments

Powered by Blogger.