Full-Width Version (true/false)


TANZANIA YATINGA FAINALI YA KOMBE LA DUNIA RUSSIAMashindano ya Kombe la Dunia la Watoto yameendelea tena leo mjini Moscow nchini Urusi katika uwanja wa klabu ya Lokomotive Moscow ambapo michezo ya nusu fainali ilichezwa ambapo Tanzania ilipambana na Uingereza na mwisho wa mchezo Tanzania imefanikiwa kutinga fainali kwa kishindo kwa kuibamiza na kuisambaratisha bila ya huruma timu ya Uingereza kwa magoli 2-1.

Mabao ya Tanzania yalifungwa na mlinzi Mastura Fadhili na Mshambuliaji Asha Omari. Tanzania itacheza fainali na Brazil kesho kutwa ambapo Brazil waliibwaga timu ya Ufilipino katika nusu fainali goli 1-0. 
Magoli ya mechi zote yalifungwa kipindi cha pili huku Tanzania wakiumiliki mchezo kwa asilimia kubwa sana na watoto wa kitanzania walionyesha umahiri mkubwa sana mbele ya Mheshimiwa Balozi wetu na wa Tanzania nchini Urusi na pia maafisa wa Ubalozi wetu walihudhuria kutazama mechi hio. 
Kwa upande mwengine John Wroe ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa wa Shirika la Street Child United lililoshiriki kuandaa mashindano haya alimpokea Mheshimiwa balozi na ujumbe wake na kumpa zawadi na kisha baada ya mechi alimpa pongezi sana kwa ushindi uliopata Tanzania leo dhidi ya Uingereza. 
Timu ya Tanzania imefika fainali tena ikiwa imeruhusu wavu wake kutikiswa mara moja tu chini ya mlinda mlango mahiri Sifaeli Geofrey na pia Tanzania inaelekea kutetea taji lake fainali kwani ndio mabingwa wa kombe hili tangu yalipofanyika mashindano haya mwaka 2014 nchini Brazil. 
Tuendelee kuiombea Tanzania ibebe tena kombe na tuendelee kuitangaza Tanzania Kimataifa zaidi. Mungu Ibariki Tanzania. Asanteni sana.

No comments

Powered by Blogger.