Tarimba anaitaka nafasi ya Manji Yanga?
Tangu aliyekuwa Mwenyekiti wa YangaYusuf Manji ajiudhulu
nafasi hiyo mwezi Mei mwaka uliopita, aliyekuwa Rais wa klabu hiyo Abbas
Tarimba amezungumzia hatma yake katika klabu hiyo ya Yanga.
Yanga imetangaza kufanya mkutano wake mkuu Juni 17 mwaka huu na jina
la Tarimba limeonekana kutawala midomoni mwa baadhi ya wanachama
wakitaka agombee nafasi hiyo.
“Wana Yanga wakinitaja kuwemo katika wale wanaofikiria wanafaa kuwa
viongozi wa klabu kwangu mimi ni heshima kubwa sana na niwashukuru
wanayanga kwa kunifikiria hivyo.”
“Niseme nimelisikia na kuliona ni jambo muhimu sana ingawa tunaita ni
fitina za kimichezo lakini mimi binafsi nalipa ukubwa sana na
ninalifikiria vizuri kwa sababu na mimi ningependa Yanga ifanye vizuri
na kama nina weza kutoa mchango kwa klabu yangu kwa nini nisifanye
hivyo?
“Kwa kuwa wanayanga wanaona naweza kuchangia kwa namna moja ama nyingine nikiwa kiongozi wao si v
No comments