Tetesi za soka balani ulaya leo Jumatano MEI 30, 2018
Manchester United na Chelsea wameonesha nia ya kutaka kumsajili Mhispania Jordi Alba mwenye umri wa miaka 29 anayeichezea Barcelona. (Sport)
Rais wa klabu inayocheza ligi ya daraja la tatu nchini Italia Rimini FC amesema yuko tayari kumchukua mlinda lango wa Liverpool Loris Karius kwa mkopo wa mwaka mzima kama zawadi yake ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ambayo ni tarehe 22 Juni. Kwa hiyo Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 24 anaweza walau "kutulia na kujiamini tena" baada ya aibu aliyoipata katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. (Rimini FC)
West
Ham wanafanya mazungumzo na Barcelona kwa malengo ya kusaini mkataba na
Mbrazili anayecheza safu ya kati- kushoto - Marlon Santos mwenye umri
wa miaka 22. (Mundo Deportivo)
The
Hammers pia wako makini kumleta mchezaji wa safu ya ulinzi wa Genoa
Mwitaliano - Armando Izzo mwenye umri wa miaka 26- katika klabu hiyo.
(Sky Sports)
Real
Madrid ndio wenye fursa zaidi ya Arsenal ya kusaini mkataba na mchezaji
wa safu ya ulinzi wa Atletico Madrid, raia wa Uruguay Jose Gimenez, na
wanatarajia kutimiza malipo yake mapya ya pauni milioni £53m .
(Talksport)
Inter
Milan watatakiwa kulipa euro milioni 40 kumchukua mchezaji wa kiungo
cha kati wa Barcelona Rafinha, mwenye umri wa miaka 25 raia wa Brazil
ambaye alikuwa kwa mkopo katika klabu hiyo ya ligi kuu ya Italia katika
msimu uliopita. (La Gazzetta dello Sport)
Rais
wa Lazio Claudio Lotito amesema kuwa alikataa kupokea euro milioni 110m
(£95.75m) ili amuuze Mserbia Sergej Milinkovic-Savic mwenye umri wa
miaka 23 anayecheza katika safu ya kati. (Football Italia)
Tottenham
wana wasiwasi kuwa matumaini yao ya kusaini mkataba na Mwingereza
anayechezea Fulham Ryan Sessegnon mwenye umri wa miaka 18 yatavurugwa na
azma ya mmiliki wa mmiliki wa Fulham Shahid Khan ya kununua uwanja wa
Wembley. (Evening Standard)
Kutoka BBC
No comments