Full-Width Version (true/false)


TFF yafuta tuzo ya mchezaji bora wa kigeni


 

Clifford Ndimbo


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limefuta tuzo ya Mchezaji Bora wa Kigeni wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambayo mwaka jana ilichukuliwa na kiungo Mzimbabwe wa Yanga, Thabani Scara Kamusiko – huku likiteua wachezaji 30 kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa ligi msimu wa 2017-2018. 

Taarifa ya TFF iliyotolewa na Msemaji wa shirikisho hilo, Clifford Ndimbo imesema kwamba shere za Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu zitafanyika Juni 23 mwaka huu ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Pia msimu huu imongezwa Tuzo ya Mwamuzi Bora Msaidizi ambayo haikuwepo msimu uliopita, hiyo ni kutokana kuthamini nafasi ya waamuzi wasaidizi.

Kwa mazingira hayo tuzo zitakazotolewa Juni 23, ni Bingwa, Mshindi wa Pili, Mshindi wa Tatu, Mshindi wa Nne, Mfungaji Bora, Timu yenye nidhamu, Mchezaji Bora chini ya umri wa miaka 20, aambayo imepewa jina la Tuzo ya Ismail Khalfan, Mchezaji Bora Chipukizi, Mwamuzi Bora Msaidizi, Mwamuzi Bora, Kipa Bora, Kocha Bora, Bao Bora Kikosi Bora cha Wachezaji 11 wa Ligi Kuu na Mchezaji wa Heshima.

Zawadi kwa kila kategori pamoja na majina ya wanaowania tuzo ukiacha bingwa, mshindi wa pili, wa tatu, wa nne na mfungaji bora ambao hujulikana kulingana na ligi inavyoendelea zitatangazwa siku za usoni.

Kamati ya Tuzo za VPL, imekamilisha orodha ya awali ya wachezaji 30 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msimu wa mwaka 2017/18, ambaao ni Habibu Kyombo (Mbao FC), Khamis Mcha (Ruvu Shooting FC), Yahya Zayed (Azam FC), Razack Abalora (Azam FC), Bruce Kangwa (Azam FC), Aggrey Morris (Azam FC), Himid Mao (Azam FC), Awesu Awesu (Mwadui FC), Adam Salamba (Lipuli FC), Mohammed Rashid (Prisons FC), Shafiq Batambuze (Singida United) na Mudathir Yahya wa Singida United.
 
Wengine ni Marcel Kaheza wa Maji Maji FC, Ditram Nchimbi wa Njombe Mji FC, Eliud Ambokile wa Mbeya City, Shaaban Nditi, Hassan Dilunga wote   wa Mtibwa Sugar, Tafadzwa Kutinyu wa Singida United, Ibrahim Ajib, Gardiel Michael, Papy Tshishimbi, Kelvin Yondani, Obrey Chirwa wote wa Yanga SC, Aishi Manula, Emmanuel Okwi, John Bocco, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Shiza Kichuya na Asante Kwasi wote wa Simba SC.

No comments

Powered by Blogger.