Full-Width Version (true/false)


Timu Zilizoshushwa Daraja Zatajwa na TFF

Ikiwa zimebakia takribani siku 22 kumaliza kwa mashindano ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa mwaka 2017/18 kwa mujibu wa kalenda, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia Bodi ya Ligi imezitangaza rasmi timu tatu kuzishusha daraja kutokana na kufanya vibaya.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura hii leo Mei 09, 2018 wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari na kuzitaja klabu hizo kuwa ni Namungo FC ya Lindi,  Pepsi FC ya Dar es Salaam, na Boma FC ya Kyela, Mbeya.

Kwa upande mwingine, Wambura amezitaja na kuzipongeza klabu sita zilizoweza kupanda daraja moja kwenda jingine ambazo ni JKT Tanzania FC ya Dar es Salaam, African Lyon ya Dar es Salaam, Kinondoni Municipal Council FC ya Dar es Salaam, Coastal Union ya Tanga, Biashara United FC ya Musoma pamoja na Alliance Schools FC ya Mwanza.

No comments

Powered by Blogger.