Full-Width Version (true/false)


TRA yajinadi kuongeza mapato


Wastani wa ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha miezi 10 ya Mwaka wa Fedha 2017/18 katika Jumuiya ya Afrika Mashariki umeongezeka hadi kufikia asilimia 16 ukilinganisha na asilimia 14 katika kipindi kama hicho cha 2016/17. 
Hayo yamesemwa na Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere baada ya kumaliza Kikao cha 44 cha Makamishna Wakuu wa Mamlaka za Mapato za Jumuiya hiyo kilichofanyika tarehe 29 hadi 30 Mei, 2018 katika Ukumbi wa Benki Kuu, Zanzibar ambacho TRA ilikuwa mwenyeji.

"Katika kikao hiki tulichomaliza leo, tumejadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mafanikio tuliyoyapata ambayo ni kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato katika Jumuiya yetu kutoka asilimia 14 kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/17 hadi kufikia asilimia16 katika kipindi kama hicho cha Mwaka huu wa Fedha wa 2017/18",  Kichere.

Kichere alieleza kuwa, pamoja na mafanikio hayo, kikao hicho kimejadili na kukubaliana masuala mbalimbali yakiwemo kuimarisha utozaji kodi kwa watu binafsi na wafanyabiashara wadogo na kuweka mipango mahususi ya kutoza kodi stahiki kutoka kwa wafanyabiashara hao.

"Pia, tumekubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano katika Mamlaka za Mapato za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kupeana taarifa na kuonyeshana mianya ya ukwepaji kodi ili kudhibiti na kukomesha hali hiyo," Kichere.

No comments

Powered by Blogger.