Full-Width Version (true/false)


TSHISHIMBI AREJEA KWAO CONGO


Akijiuguza kwa muda wa wiki mbili bila matarajio ya kupona, kiungo mkabaji wa Yanga Mkongoman, Papy Kabamba Tshishimbi ameamua kurudi kwao fasta kwa ajili ya kwenda kujitibia kwa miti shamba.

Kiungo huyo yupo nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili akiuguza majeraha yake ya enka aliyoyapata katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika walipokutana na Wollayta Dicha ya Ethiopia na hata kwenye mchezo dhidi ya Rayon Jumatano, hatakuwepo.

Staa huyo aliyewabamba mashabiki wa Yanga, hadi sasa amekosa mechi mbili dhidi ya USM Algier’s na ile ya Prisons na hata ya leo Jumapili na Mtibwa mjini Morogoro ataikosa.

Habari za ndani zinasema kwamba amerudi kwao baada ya kutoridhishwa na matibabu aliyokuwa akipata hapa nchini na amewaambia viongozi kuwa kuna sehemu kule kwao anaweza kupata dawa za kienyeji zikamrudisha kwenye hali nzuri.

Kocha wa Yanga, Zahera Mwinyi alipoulizwa kuhusu mchezaji huyo alisema; “Ni kweli Tshishimbi hayupo na timu ana majeraha ya enka aliyoyapata katika mechi za nyuma. Yeye hayupo katika timu kwa muda wa siku nne akiendelea na matibabu.”

No comments

Powered by Blogger.