Full-Width Version (true/false)


"Tunda Man mdogo sana"- Bob JuniorMsanii na muandaaji wa muziki Bob Junior amesema kuwa Tunda Man amemzidi umri tu lakini kwenye kazi yeye ni mkubwa zaidi yake. 
Bob Junior amesema hayo kupitia eNews ya EATV huku akisisitiza kuwa muziki ameanza muda mrefu lakini wazazi walikuwa wakimzuia na kusisitiza asome kwanza kwa kuwa alikuwa bado mdogo.

“Tunda ni kaka yangu na nina mheshimu kwakuwa kanizidi umri na baadhi ya vitu lakini kwenye kazi tuheshimiane mie sio mtoto kama anavyosema mbona nmemfanyia baadhi ya nyimbo zake tena bure wakati anaanza, sasa nani mdogo hapo kati yetu”,  amesema Bob Junior.

Hayo yamejiri baadaya msanii Tunda Man kutoa 'video' tatu za nyimbo zake mpya suala ambalo lilimuibua Bob Junior na kutoa ushauri kwa msanii huyo kuwa alitakiwa kutoa kwa awamu ili awape muda mashabiki wake.

No comments

Powered by Blogger.