Full-Width Version (true/false)


"Tupo tayari hata miaka 10 ijayo" Ole SosopiMwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA, Patrick Ole Sosopi ameweka wazi kuwa wao kama Chama cha Demokrasia na Maendeleo wapo tayari kuongozwa na Mbowe katika safari ya mapambano ya chama chao hata kwa miaka 10 ijayo. 
Akizungumza kwenye kipindi cha  Kikaangoni kinachorushwa kila Jumatano kupitia ukurasa wa Facebook EATV amesema kuwa CHADEMAkuongozwa na Mbowe ni maamuzi ya wanachadema wala siyo maamuzi ya wana CCM wala chama kingine.

Ameongeza "Kwenye vyama vyetu vya upinzani Sisi hatuchagui kiongozi peke yake, tunachagua watu wanaoweza kuongoza mapambano. Sisi tupo kwenye hiki chama na Mbowe yupo kwenye chama anaongoza mapambano".

Amesisitiza "Hatubadilishi kama ambavyo CCM haijawahi kubadilisha kama ambavyo CCm haibadilishi. CCM haijawahi kubadilishaMwenyekiti kwani kuwa kiongozi wa nafasi hiyo lazima uwe rais wa chama hicho. Mimi mwenyewe nastahili kuwa Mwenyekiti. Katika kipindi hiki Mbowe ndiye anayetuongoza mpaka tufikie malengo".

No comments

Powered by Blogger.