Full-Width Version (true/false)


Tuweke maneno pembeni, Alikiba ameni-inspire kwa kinywaji – Nandy

Hitmaker wa ngoma ya Kivuruge, Nandy amesema hatua aliyopiga Alikiba kwa kuingiza sokoni bidhaa yake ya energy drink ni moja ya vitu ambayo vimemuhamasisha kufanya vitu vikubwa.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma ‘Ninogeshe’ ameiambia The Playlist ya Times FM kuwa hivyo ni vitu ambavyo wasanii wa sasa wanapaswa kuiga, yaani kuwekeza nje ya muziki.
“Tuweke maneno pembeni, kwa kweli nilivyoona alivyotambulisha kinywaji chake alini-inspre kutoka moyoni mwangu,” amesema Nandy.

“Ameni-inspire kwa kinywaji kwa sababu ukiangalia the parkage ya kinywaji chake jinsi ilivyo ni project fulani ambayo ipo serious,” amesisitiza.

Muimbaji huyo aliendelea kwa kusema si Alikiba pekee amevutiwa naye katika kuwekeza nje ya muziki bali hata Diamond Platnumz.

“Tunaambiwa nje ya kuimba tunatakiwa tuwekeze nje ya muziki wetu na ndicho hiki kaka zetu wanafanya ukimuangalia kama Diamond, Alikiba ni vitu ambavyo wanatuhamasisha,” amesema.
Utakumbuka usiku wa April 29, 2018 wakati wa harusi ya Alikiba ndipo hitmaker huyo wa ngoma ‘Seduce Me’, Alikiba alitangaza ujio wa bidhaa yake ya energy drink, MO FAYA.

No comments

Powered by Blogger.