Full-Width Version (true/false)


" Ubunge CHADEMA unanunuliwa kwa milioni 1"-Musukuma


Mbunge wa GeitaVijijini, Joseph amefunguka na kusema kuwa hawezi kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo kwa kuwa ni genge la wahuni na kwamba ndiyo maana Wabunge wa Viti maalumu mpaka wakubali kulipia milioni 1 kila mwezi na wale wa kuchaguliwa lazima walipie laki 5. 
Musukuma ameyasema hayo alipokuwa KIKAANGONI  East Africa Television, na kusema kwamba hakuna kitu kinachomvutia CHADEMA na hawapendi kwa sababu katika ilani na matendo yao ni vitu tofauti.

"Sisi tunaojua Wabunge wanachangishwa milioni 1 hawa wa viti maalumu. ili upewe Ubunge CHADEMA lazima usaini mkataba kwamba kila mwezi lazima ukatwe milioni moja kwa ajili ya kujenga chama. Hawa wa majimbo wanatoa laki tano, anakula Mbowe. Ningekuwa mimi mjuaji tayari ningeshampiga ngumi siku nyingi" Musukuma.

Mbali na hayo Msukuma ameongeza kwamba siku akifukuzwa CCM hawezi kwenda chama kingine kwani anaamini hakuna chama kitakachomuweza.

"Nikitolewa nitakaa nyumbani, sitahama chama, hakuna chama kinachoniweza zaidi ya CCM, ningekuwa CHADEMA kila siku wangeamua ngumi"

Mbali na hayo amesema viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakikosoa na kupinga kila kitu ndani ya bunge na kwamba wao hakuna jambo jema ambalo wanaweza kusifia.

No comments

Powered by Blogger.