Full-Width Version (true/false)


Ufinyu wa Bajeti waikabili Wizara ya UlinziWaziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, amesema, ufinyu wa Bajeti ya Wizara hiyo, umesababisha kulegalega kwa utoaji wa huduma na Wizara kuendelea kuwa na madeni ambayo yanaathiri utendaji na kupoteza uaminifu kwa wazabuni wanaotoa huduma. 
Dk. Mwinyi ametoa kauli hiyo Bungeni wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2018/19 ambapo amesema, kiwango kilichoidhinishwa cha shilingi trilioni 1.7 ni kidogo ambapo mahitaji halisi ni shilingi trilioni 3.2.

Pamoja na hayo Dk Mwinyi amesema hadi kufikia Aprili mwaka huu, wizara ilikuwa imepokea Sh 181.58bilioni sawa na asilimia 82.91 bilioni kati ya Sh 219 bilioni zilizoidhinishwa na bunge katika bajeti ya 2017/18 kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo.

Kwa upande wake Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, ikiwasilisha maoni yake kupitia Makamu Mwenyekiti wake, Salum Rehani, imeishauri serikali kuona umuhimu wa kuongeza ukomo wa bajeti ya Wizara kulingana na mahitaji yake halisi ili kuliongezea jeshi uwezo wa kiutendaji.

No comments

Powered by Blogger.