Full-Width Version (true/false)


Ugonjwa wa kifua kikuu bado ni tishio nchini.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema ugonjwa wa kifua kikuu bado ni tishio kubwa kwa watu wazima na watoto kufuatia takwimu za osi ya takwimu ya taifa (NBS) kuonyesha kuwa takribani watu 65, 000 hapa nchini wanaugua ugonjwa huo kila mwaka. 

Mratibu wa kifua kikuu na Ukimwi kutoka Wizara ya Afya, WANZE KOHI akizungumza na watumishi zaidi ya 120 wa sekta ya Afya kutoka mikoa ya kanda ya ziwa katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wa utambuzi wa ugonjwa wa kifua kikuu kwa watoto ametoa rai kwa jamii kutokuogopa kupeleka watoto wao katika vituo vya kutolea huduma za Afya ili kupatiwa matibabu mapema kwani matibabu ya ugonjwa huo ni bure. 

Mwezeshaji wa mafunzo hayo, ambaye pia ni mratibu wa kudhibiti kifua kikuu na Ukoma mkoa wa Shinyanga Dkt. JOHN MAJIBWA, amesema kuwa tatizo ni kubwa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, huku mratibu wa kifua Kikuu na Ukoma mkoa wa Dar es Salaam Dkt. MRISHO LUPINDA akisema mkoa huo ndio unaoongoza nchini kwa kuwa na wagonjwa wengi wa kifua kikuu. 

Baadhi ya Maasa Tabibu kutoka kituo cha Afya Kamachumu wilaya ya Muleba mkoani ya Kagera pamoja na kituo cha Afya Kasuguti wilayani Bunda mkoani Mara wamesema mafunzo hayo yatawasaidia katika kutibu ugonjwa huo wa kifua kikuu kwa watoto wachanga.

No comments

Powered by Blogger.