Full-Width Version (true/false)


Uhamiaji Yakamata Wakazi 1200 Wanaoishi bila Kibali Nchini


Idara ya Uhamiaji Wilaya ya Tarime imebaini uwepo wa wananchi 1200 ambao wanaishi nchini kinyume cha sheria.

Mratibu wa uhamiaji wilaya Tarime mkoani Mara,Mbaraka Haji Batenga aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake kuwa idara yake imefanya upembuzi akinifu na kubaini kuwa kuna watu 1200 wanaishi wilayani hapa kinyume cha sheria bila kufuata utaratibu.

Batenga aliongeza kuwa idara hiyo inafanya mchakato wa nini cha kufanya juu ya wakazi hao pamoja na kuandaa fomu maalumu inayoambatana na kiapo kwa  kila moja kujaza ili kutambuwa kazi yake pamoja na mahala anapokaa.

Afisa huyo aliwaomba wanachi pamoja na viongozi ngazi ya mtaa,vijiji,na kata kutoa ushirikiano wa kuwabaini wageni wasiokuwa wakazi halali wa Tanzania.

"Tumewatambua  watu 1200 ambao sio watanzania na wanaishi hapa kinyume cha sheria ambapo hatua zinafanywa ili kuwachukulia hatua watu hao ikiwa ni pmoja na kuandaa fomu maalumu ya kila mkazi asiye kuwa raia wa Tanzania kujaza mahali anapokaaa pamoja na shuguli anayofanya kazi ambayo itafanywa na viongozi mbalimbali wa seriklai ikiwemo wale wa mitaa,vitongoji,vijiji na kata"alisema Batenga. 

Batenga alibainisha kuwa wageni waliobainishwa ni pamoja na wanawake walioolewa kuja Tanzania pamoja na wanaume ambao wamehami kuja kuishi na kufanya shuguli za uzalishaji.

Nchi yetu ni nchi ya utaratibu kwa hali hiyo kuna haja wageni kutambuliwa na kuwa ili kuwatambua wageni kunasiri kubwa ndani yeke kwasababu wengi wanakuja na kuchukua haki za Watanzania na kufanya hiyo tunalinda haki za watanzania zisichukuliwe na wageni aliongezakusema Batenga

No comments

Powered by Blogger.