Full-Width Version (true/false)


Ukitaja wasanii 10 duniani wenye sauti nzuri, Diamond huwezi kumtoa-Waziri MwakyembeWaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa ukitaja majina ya wasanii 10 wa muziki duniani wenye sauti nzuri za kuimba huwezi kuacha kutaja jina la msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz.
Waziri Mwakyembe

Mwakyembe amesema hayo kwenye mahojiano yake na kipindi cha KAA HAPA cha Mrisho Mpoto na kueleza kuwa Diamond kwenye video zake hana haja ya kutumia picha za ajabu ajabu kwani sauti yake ni dhahabu inajiuza.

Kwenye tasnia yetu ya sanaa  vijana wetu wanaimba nyimbo nzuri sana, wana vipaji vya hali ya juu. kinacholeta matatizo hapa ni  picha ambazo haziendani na maadili yetu, kuchanganya na utupu ndani yake hivi vitu kwa kweli wafanye wengine lakini sio hapa. Tuchukulie kijana kama Diamond sauti yeke pekee yake inatosha kabisa kumuuza. Ukisema wasanii 10 duniani tuwe wakweli tuu! wenye sauti nzuri, Diamond huwezi kumtoa pale. Lakini huitaji kuuza ukaongeza na picha za ajabu ajabu wanaofanya hivyo ni wale wenye mapungufu ili kuficha ma’flat flat kwenye nyimbo zao Diamond yeye haitaji kufanya hivyo.“ameeleza Waziri Mwakyembe alipoulizwa sababu za kumsamehe rapa Roma Mkatoliki ile hali walitangaza kumfungia .
Hata hivyo, Mwakyembe amesema kuwa serikali haina tatizo wala ugomvi na wasanii wa Tanzania bali kilichopo ni jitihada za dhati za kulinda maadili ya Mtanzania, ndio maana serikali imekuwa ikifungia baadhi ya nyimbo za wasanii na kusisitiza kuwa nyimbo zote zilizofungiwa hazitafunguliwa kwa matumizi ya umma mpaka zibadilishwe baadhi ya mashairi na picha.

Mwezi Machi, Serikali kupitia Baraza la Sanaa Taifa, ilitangaza kumfungia rapa Roma Mkatoliki kutokujihusisha na muziki kwa miezi sita lakini wiki mbili baadaye ikatangaza kumfungulia adhabu hiyo.

No comments

Powered by Blogger.