Full-Width Version (true/false)


Ukiwa “single” utaishi miaka mingi
Kikongwe wa miaka 106 Madeline Dye, raia wa Uingereza, amebainisha kuwa siri kubwa ya kuishi miaka mingi ni kutoingia katika mahusiano ya kimapenzi na kutoenda pub. 
Madeline hajawahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mwanaume yeyote na aliingia pub katika sherehe ya siku yake ya kuzaliwa alipofikisha umri wa miaka 90.

Kikongwe huyo amesema kwamba anadhani ameishi muda mrefu kwasababu ameepuka msongo wa mawazo “stress” kuwa katika mahusiano ya mapenzi na akiulizwa sababu ya kuishi muda mrefu amekuwa akisema ni kuwa single.

Madelina alizaliwa April 28, 1912 katika mji wa Sheffield na ameendelea kuishi katika mji huo maisha yake yote baada ya baba yake kufariki katika vita ya kwanza ya Dunia 1918.

Kwa mujibu wa utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Harvard nchini Marekani umebainisha kuwa tabia za mtu kuweza kuishi muda mrefu ni kula mlo kamili, kufanya mazoezi, kutokunywa pombe au kuvuta sigara na kuepuka uzito uliopitiliza.

No comments

Powered by Blogger.