Full-Width Version (true/false)


Ulimboka aitaka Simba kuacha usajili wa pupa 

Mshambuliaji wa zamani wa Taifa Stars na Simba, Ulimboka Mwakingwe amewashauri waajili wake wa zamani kuacha kutumia fedha vibaya katika usajili badala yake wawe makini ili waweze kufikia mafanikio.

Simba sasa ni klabu yenye uwezo wa kusajili mchezaji yeyote kutokana na kupitisha katiba mpya ambayo inawafanya waendeshe timu yao katika mfumo wa kampuni.

Ulimboka alisema amekuwa akifuatilia usajili wanaoufanya na umekuwa ukimshangaza kutokana na kusajili vijana wengi ambao hawawezi kuwasaidia kimataifa kutokana na kukosa uzoefu.

"Sina sababu ya kuzuia usajili wao ila natoa maoni ya yangu naona kama Simba hawana mapungufu mengi hivyo umakini unatakiwa ikiwa ni kuhakikisha wanafuata ripoti ya mwalimu," alisema winga huyo wa zamani wa Mtibwa.

Mwakingwe alitolea mfano safu ya ushambuliaji ambapo alisema hakuna tatizo kubwa, lakini wanatakiwa kuongeza wachezaji wawili walio na uwezo zaidi ya Emmanuel Okwi na John Bocco ambao watawapa changamoto nyota hao.
     

No comments

Powered by Blogger.