Full-Width Version (true/false)


Unai Emery kukabidhiwa mikoba ya Wenger wiki hiiKlabu ya Arsenal inatarajia kumtangaza wiki hii aliyekuwa meneja wa Paris Saint-Germain, Unai Emery kurithi mikoba ya Arsene Wenger.
Emery ambaye ameachana na klabu ya PSG mwanzoni mwa mwezi huu ameonekana katika Jiji la London hapo jana siku ya Jumatatu akifanya mazungumzo na the Gunners.

Kocha huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 46, ameongoza klabu ya PSG ya nchini Ufaransa na nafasi yake kuchukuliwa na Thomas Tuchel.

Chanzo kimoja kilichopo karibu na mazungumzo hayo kimeeleza kuwa Emery ndiye kocha pekee aliyepewa nafasi ya kuchukua mikoba ya Arsene Wenger.

No comments

Powered by Blogger.