Full-Width Version (true/false)


Unalalamika Hela za Rambirambi Umechangia Nini?- Steve Nyerere

Muigizaji wa Bongo Movie Steve Nyerere amezungumza kuhusu watu wanaolalamika kuwa yeye na baadhi ya watu waliokuwa kwenye kamati ya mazishi ya msiba wa Masogange wamekula za rambirambi ambapo Steve amedai kuwa anashangaa sana watu kwenda kulalamika mitandaoni kuhusu hela hizo wakati mtu huyo hajatoa kitu zaidi ya kuvaa sare na kulia.

Steve Nyerere amesema hela ya rambirambi ipo ambayo ni Milioni 2 na laki moja lakini kama kamati walikubaliana kumuwekea mtoto ije imsaidie kwenye masomo yake na watu wanao lalamika kuwa hela zimeliwa hawajatumia ustaarabu kwenda kulalamika kwenye mitandao wakati wao hawajajitoa chochote.

“Sizani kama mtu mwenye akili timamu tena kama wewe ni ndugu ambae hata arobaini ya marehemu haijafika unafikia muda unaanza kuongelea michango iliyobaki ndani akili yako yote ilitakiwa iende kwenye arobaini,”

Niulize unatokaje kwenda kuzungumza kwneye vyombo vya habari wewe umechangia nini zaidi ya kulia? umechangia jeneza?” – Steve Nyerere

No comments

Powered by Blogger.