Full-Width Version (true/false)


UONGOZI YANGA WAOMBWA KUIGA JAMBO HILI KUTOKA SIMBAKufuatia kushindwa kufanya hivi karibuni na licha ya kikosi cha Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao FC katika mchezo wa ligi uliopigwa jana Uwanja wa Taifa, mashabiki Yanga wameutaka uongozi wao kufanya mabadiliko.

Mapema baada ya mchezo dhidi ya Mbao kumalizika, baadhi ya wapenzi, mashabiki na wanachama walitoa maoni yao kuhusiana na mwenendo wa kikosi cha Yanga wakieleza ni vema Yanga ikaiga walichofanya Simba.

Wengi walieleza ni wakati mwafaka sasa kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshwaji wa klabu hiyo ili kuepukana na kuyumba kwa uchumi, suala ambalo klabu inalipitia kwa sasa.

Mbali na hilo mashabiki hao wameeleza kuwa mfumo uliopo hivi sasa umesababisha Yanga kuwa na matatizo haya yanayoikumba hivi sasa haswa ukata wa fedha huku wakishauri ni muda sahihi kuondokana nao.

Wakati mashabiki hao wakitoa maoni hayo, watani zao wa jadi Simba tayari wameshakamilisha mchakato mzima na kilichosalia hivi sasa ni usajili wa katiba na uwezekano mkubwa wa mfumo huo kuanza kutumika upo kabla ya msimu ujao wa ligi kuanza.

No comments

Powered by Blogger.