Full-Width Version (true/false)


Usari kidigitali kama uber watinga Mwanza

 
WANANCHI na madereva 'tax 'wa mkoa wa Mwanza, wamehimizwa kuchangamkia fursa mpya ya usafiri wa kidijitali ( mtandao) ya Taxify . 

Akizungumza katika uzinduzi wa huduma hiyo Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Mary Onesmo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo, John Mongella, alisema huduma hiyo itapunguza gharama na muda wa kusafiri. 

"Taxify itaongeza ajira na kipato kwa madereva teksi jijini Mwanza na unafuu wa nauli kwa abiria watakaoita usafiri kupitia simu za mkononi popote walipo," alisema. 

''Cha msingi ni kuikamata fursa hiyo na watambue kuwa huduma hiyo itanufaisha watu wengi wakiwamo wenye ulemavu na wazee waliokuwa wanataabika kutembea umbali mrefu kutafuta usafiri wa teksi,'' alisemaKwa upande wake, Ofisa Uendeshaji Taxify Mwanza, Milumbilwa Kipimo aliwataka madereva teksi kujisajili na kwamba kampuni hiyo itatoa punguzo la asilimia 50 ya gharama ya usafiri kwa abiria kati ya Mei 28 na Juni 30, mwaka huu. 

"Gharama ya usafiri kwa kipindi hiki ni Sh 700 kuanza safari, Sh 460 kwa kilomita moja na Sh 70 kwa dakika moja," alifafanua Ofisa Uendeshaji Taxify Tanzania, Remmy Eseka alisema jiji la Mwanza ni pili kufikiwa na kampuni hiyo nchini, likitanguliwa na Dar es Salaam ambako ilianza kutumika mwaka 2017 lakini Taxify inaunganisha watumiaji na watoa huduma ya usafiri ulimwenguni kote. 

Mwenyekiti wa madereva teksi Mwanza, Beatus Mirambo alisema wameipokea Taxify lakini elimu ya huduma ya usafiri kidijitali inahitajika kwa wadau, ingawa kuna changamoto kwa baadhi ya madereva na abiria kutokuwa na simu zenye uwezo wa kuingia kwenye mtandao (smart). 

Msanii wa muziki wa hiphop, Fareed Kubanda a.k.a Fid Q akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya Taxify iliyofanyika hivi karibuni jijini Mwanza.

No comments

Powered by Blogger.