Full-Width Version (true/false)


Vanessa Mdee afanya kazi na producer wa Michael Jackson na Celine Dion

Vanessa Mdee amekuwa akipambana kwa kila hali kuhakikisha muziki wake unafika mbali zaidi. Msanii huyo amekutana na producer na audio engineer, Humberto Gatica ambaye ni mshindi wa tuzo 16 za Grammy na kufanya naye kazi.


Vanessa Mdee akiwa na Humberto Gatica

Vanessa amekutana na producer huyo katika studio maarufu duniani ya Abbey Road iliyopo nchini Uingereza na kutengeneza project ya kazi kwa ajili ya tamasha la Bantu Jazz litakalofanyika Juni 9 ya mwaka huu nchini Garbon.Akiongea na mtangazaji Fredrick Bundala, Vee Money amesema kuwa Gatica pia atakuwepo kwenye tamasha hilo litakalofanyika Garbon.

Gatica amewahi kufanya kazi na wasanii wakubwa duniani akiwemo Barbra Streisand, Mariah Carey lakini kubwa zaidi ni Thriller ya Michael Jackson, My Heart Will Go On ya Celine Dion na nyingine.

No comments

Powered by Blogger.