Full-Width Version (true/false)


Vanessa Mdee na Jux waja na tour yao, wataja kiingilio na kituo cha runinga kitakachorusha live show zao

 

Wasanii wawili wa muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee na Jux wametangaza rasmi ziara yao ya muziki nchini Tanzania waliyoipa jina la ‘In Love & Money Tour’ ambapo wapenzi hao watazunguuka mikoa minne Tanzania bara.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kwenye uzinduzi wa Tour hiyo, Vanessa Mdee amesema huu ni wakati muafaka kwa mashabiki wake na Jux kuwaunga mkono kwani tangu waanze mahusiano yao hawajawahi kupanda jukwaa moja nakuimba.

Naye, Jux amesema kuwa show zao zote zitakuwa na kiingilio sawa cha Tsh 5,000/= na wataanzia jijini Mwanza tarehe 30 mwezi Juni mwaka huu.

Jux amesema show zote za ziara hiyo zitaoneshwa Live kupitia Clouds Plus huku Vanessa Mdee akiahidi kutumbuiza nyimbo zake zote zilizopo kwenye album yake ya Money Mondays.

No comments

Powered by Blogger.