Full-Width Version (true/false)


Vijana kuna kazi azihitaji uzoefu, unaweza ukagombea Udiwani na Ubunge – Spika NdugaiSpika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amewataka vijana nchini kugombea nafasi ambazo hazihitaji uzoefu kama udiwani na Ubunge.

Spika Ndugai amesema hayo Bungeni leo, Mei 18, baada majibu ya Mbunge wa viti maalumu Zainab Katimba kutaka kujua mkakati wa Serikali katika kutatua tatizo la ajira kwa vijana wasomi wasio na uzoefu(Work Experience).

“Asante sana Waziri wa nchi kwa majibu ya nyongeza, eeh Vijana wasomi, zipo kazi nyingine hazihitaji uzoefu, mnagombea Udiwani, mnagombea Ubunge, nawatangazia vita waheshimiwa hapa,” Spika Ndugai alitoa kauli hiyo akicheka.

Aidha serikali imesema imetafuta ufumbuzi wa tatizo la uzoefu wa ajira kwa kushirikiana na Waajiri, vyama vya wafanya kazi kwa kutafuta Makampuni mbalimbali ili vijana waende kusoma na kujipatia vyetu vya uzoefu ili kuepuka usumbufu wakati wa kutafuta ajira.

No comments

Powered by Blogger.