Full-Width Version (true/false)


''Vijana wa UVCCM wanajipendekeza'' - SosopiKupitia kipindi cha KIKAANGONI cha East Africa Television Mei 16, 2018, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) Patrick Ole Sosopi, amesema vijana wa UVCCM wanafanya mambo kwa kujipendekeza ili wateuliwe. 
Sosopi amesema vijana wa BAVICHA wanafanya kazi ya kujitolea kutetea mambo mbalimbali nchini ikiwemo demokrasia na amani, kwasababu hawana malipo tofauti na UVCCM ambao wanafanya mambo kwa kujipendekeza ili wateuliwe kwenye nafasi mbalimbali serikalini.

''Kuna tofauti kubwa kati ya vijana wa CHADEMA na CCM kwasababu sisi hatuna mtu wa kumfurahisha, utamfurahisha Mwenyekiti Mbowe ili akupe nini, kwetu hakuna nafasi za uteuzi lakini wenzetu wanatazama kuwa DC, RC au DED'', ameeleza.

Sosopi ameongeza kuwa kitu pekee ambacho kina mjenga kijana wa BAVICHA ni 'struggle'. ''Ili uwe mbunge au kupata nafasi yoyote ndani ya Chama ni lazima 'ustruggle' hakuna njia nyingine''.

No comments

Powered by Blogger.