Full-Width Version (true/false)


VITA KUBWA LEO NI REAL MADRID VS LIVERPOOL KATIKA USIKU WA FAINALI ULAYA


Vita kubwa iliyokuwa inasuburiwa kwa hamu ya fainali ya Mabingwa Barani Ulaya inashika kasi usiku wa leo nchini Ukraine katika Uwanja wa Olimpiyskiy National Sports Complex ambapo Real Madrid na Liverpool zinakutana.

Real Madrid walitinga hatua hiyo ya fainali baada ya kuwoandoa Juventus huku Liverpool wakitoa AS Roma ya Italy.

Kuelekea mechi hiyo, nyota wawili ndiyo wanaozungumziwa zaidi hivi sasa ni Cristiano Ronaldo na Mohamed Salah wanaopewa nafasi kubwa ya kuzibeba timu zao.

Ronaldo amekuwa hana msimu mzuri nchini Spain na Madrid katika La Liga wakati huo nyota Mmisri, Salah amekuwa na mwaka mzuri kwa kutwaa tuzo kibao ikiwemo ya mchezaji bora nchini England msimu huu.

Mechi hii inayotarajiwa kuanza majira ya saa 3 na dakika 45 usiku inasubiriwa na wadau wengi wa michezo duniani ambao wana shauku kubwa ya kuona nani atalibeba taji hilo kubwa duniani.

No comments

Powered by Blogger.