Full-Width Version (true/false)


VITA YA EL CLASICO YAKOSA MBABE, MECHI YAMALIZIKA KWA SARE

Vigogo wa soka nchini Spain, FC. Barcelona na Real Madrid zimetoshana nguvu katika Uwanja wa Camp Nou kwa mchezo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Ilikuwa ni Barcelona iliyoanza kujipatia bao la kwanza kupitia kwa Luis Suarez aliyefunga katika dakika ya 10 ya mchezo huku la pili likitiwa kimiani na Lionel Messi dakika ya 52.

Real Madrid walijipatia mabao yao kupitia kwa Cristiano Ronaldo katika dakika ya 14 na Gareth Bale akitumia mnamo dakika ya 72.

Barcelona walicheza kipindi cha pili wakiwa pungufu baada ya Sergi Roberto kula umeme wa kadi nyekundu mwishoni mwa kipindi cha kwanza.

No comments

Powered by Blogger.