Full-Width Version (true/false)


Vitu vitano vya kufahamu kabla ya fainali ya UEFA, Real Madrid vs Liverpool leo


Bado saa kadhaa tuweze kushuhudia fainali ya UEFA Champions League inayozikutanisha timu za Real Madrid ya Hispania dhidi ya Liverpool ya England ambapo wanacheza mchezo huo wa fainali Kyiv nchini Ukranine katika uwanja wa wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 70000.

1- Real Madrid na Liverpool wamekutana mara 4 toka February 25 2009, Real Madrid akifanikiwa kushinda mara mbili katika michezo ya hatua ya makundi wakati Liverpool na akiifunga Real Madrid mara mbili katika michezo ya hatua ya 16 bora February 25 2009 na March 10 2009.

2- Kingine cha kuvutia ni kuhusiana na kauli kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania na club ya Real Madrid Vicente del Bosque ambaye amesema hakuna mchezaji hata mmoja wa Liverpool unaeweza kumlinganisha na mchezaji wa Real Madrid.

3- Wachezaji Mohamed Salah wa Liverpool na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ndio vivutio zaidi na kila mmoja anatamani kuona ni mchezaji gai atafanya maajabu zaidi ya mwenzake usiku wa leo, Ronaldo na Salah wote wamefunga jumla ya magoli 44 msimu huu ila Salah amecheza mechi nyingi zaidi ya Ronaldo.

4- Staa wa Liverpool Mohamed Salah ambaye ni muumini wa dini ya kiislamu licha ya kuwa na msimamo wa dini yake lakini leo ameridhia kutofunga Ramadhani kutokana na mchezo huo.
5- Kama Real Madrid watachukua Kombe hilo kwa mara ya tatu mfululizo leo kocha wao Zinedine Zidane ndio atakuwa kocha wa kwanza kuwahi kutwaa taji la UEFA Champions League mara tatu mfululizo.

No comments

Powered by Blogger.