Full-Width Version (true/false)


WAAMUZI WATAKAOCHEZESHA MCHEZO WA KOMBE LA SHIRIKISHO, YANGA VS RAYON SPORTS WATAJWA


Clifford Ndimbo
 
Shirikisho la Soka nchini (TFF) limetaja majina ya Waamuzi watakaosimamia mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga dhidi ya Rayon Sports kutoka Rwanda.

Afisa Habari wa TFF, Clifford Mario Ndimbo, ametaja majina ya Waamuzi hao wanaotokea Angola.

Waamuzi ni Helder Martins Rodrigues De Carvalho (Mwamuzi wa Kati) Ivanildo Meireles De O Sanche Lopes (Mshika Kibendera namba 1), Wilson Valdmiro Ntyamba (Mshika Kibendera namba 2), Joao Amado Muanda Goma (Fourth Official) wote wakitokea Angola.

Maafisa wengine ni Abebe Solomon Gibresilassie (Commissioner) (Ethiopia), Yoland Mavouroulou (General Coordinator) (Gabon) na Clifford Mario Ndimbo ( Media Officer) Tanzania.


Mechi hiyo ya pili kwa Yanga na Rayon katika hatua ya makundi ya michuano hiyo itapigwa Mei 16 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

No comments

Powered by Blogger.