Full-Width Version (true/false)


Waarabu waharibu mipango ya YangaWakati Yanga wakiondoka nchini jana kuelekea Algeria kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya U.S.M Alger, inaelezwa kuwa mashushushu wa timu hiyo walikuwa jijini Dar es Salaam kuwafuatilia.

Alger walituma watu maalum waliokuja nchini kuitazama Yanga ilipokuwa inakipiga dhidi ya watani zao wa jadi Simba kwenye mchezo wa ligi uliopigwa Aprili 29 Uwanja wa Taifa.

Ujio wa watu hao maalum waliokuja kuchunguza mbinu za Yanga, unaweza kuwa faida kwa Waarabu hao ambao watakuwa wenyeji katika mechi hiyo itakayopigwa Mei 6 mjini Algiers.

Tayari kikosi cha Yanga kipo njiani hivi sasa kuelekea Algeria ambapo kitapitia Dubai kabla ya kuwasili nchini humo.

No comments

Powered by Blogger.