Full-Width Version (true/false)


“Wabakaji wasifungwe jela”-Mwanaharakati


Mwanaharakati wa haki za wanawake, Germaine Greer (79) kutoka nchini Australia amesema kwamba watu ambao wanapatikana na hatia kwa kosa la kubaka hawapaswi kupelekwa gerezani bali wanatakiwa kupewa adhabu ya kufanyakazi za kijamii. 
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail, mwanaharakati huyo amesema hayo jana Mei 30, 2018 akiwa Nchini Wales na kuongeza kuwa ubakaji halitakiwi kuwa kosa la jinai kwasababu wanaofanyiwa ubakaji wengi hawapati majeraha ya kimwili.

Mwanaharakati huyo ameongeza kuwa wanaopatikana na hatia kwa kosa la ubakaji wanapaswa kuchorwa alama ya R katika mkono au shavuni na kisha kutumikia adhabu kwa kufanya shughuli za kijamii kwa saa zisizopongua 200.

“Ningependekeza labda wangechorwa tattoo ndogo ingekuwa kitu kizuri, labda herufi R katika mkono au katika shavu,na kufanyakazia za kijamii kwa saa 200 ningependekea hivyo” amesema Germaine

Mwanamama huyo amedai kwamba alibakwa akiwa na umri wa miaka 18 na kuongeza kuwa hakuripoti tukio hilo Polisi kwasababu alihisi angepoteza muda wake mwingi na pia ilikuwa ni fedheha kusema hadharani kwamba amefanyiwa kitendo hicho.

No comments

Powered by Blogger.