Full-Width Version (true/false)


Wabunge Rwanda waruhusu bunduki kuuzwa dukani.


 


Wabunge nchini Rwanda kwa pamoja wamepitisha Sheria inayoruhusu bunduki kuuzwa dukani pamoja na uwepo wa viwanda vya kutengeneza aina mbalimbali za silaha.
Akifafanua mswada wa sheria hiyo kabla ya kupitishwa bugeni,Waziri wa Katiba na sheria Bw: Evode Uwizeyimana, amesema mswada huo una lenga kulinda hadhi ya nchi.
Wabunge wamepitisha mswada huo huku nchi hii ikiwa imesheheni wakazi wengi wenye itikadi za mauaji ya kimbali na  wengi wamehoa kwamba huenda bunduki hizo zikatumika kinyume na sheria. 
Lakini serikali kupitia Wizara ya sheria inasema kwamba, bunduki hazitouzwa kama karanga na mtu atakayekubaliwa kumiliki silaha, atachunguzwa vilivyo. 
Mswada wa sheria hiyo unaruhusu mtu kuanzisha kiwanda kinachotengeneza silaha na pia unaruhusu wafanyabiashara kufungua maduka ya kuuza bunduki. Rwanda inakaribia kuruhusu watu kumiliki silaha huku baadhi ya nchi kama marekani ambapo pameshuhudiwa vifo vingi vinavyotokea baada ya watu kupigwa risasi pakitolewa wito wa kubadili sheria ya kumiliki bunduki.     

No comments

Powered by Blogger.