Full-Width Version (true/false)


Wachezaji Singida United waula, kila mmoja abeba mifuko 50 ya saruji
Huku wakijiandaa kucheza fainali ya Kombe la FA dhidi ya Mtibwa Sugar, uongozi wa Singida United umemzawadia kila mchezaji mifuko 50 ya cement.


Timu hizo zinatarajiwa kuvaana keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha saa kumi kamili jioni.


Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Singida United, Festo Sanga alisema wamewapa zawadi hizo wachezaji kama sehemu ya pongezi kutokana na kuifikisha timu hiyo hapo ilipo.


“Tuna kila sababu ya kuwapongeza wachezaji wetu na viongozi kwa ujumla kwa jitihadi kubwa waliyoifanya ya kuipambania timu yao ambayo keshokutwa itacheza fainali ya Kombe la FA.“Hivyo, kama uongozi tumeona tuwazadie wachezaji wetu pamoja na viongozi wao wote kuwapatia mifuko 50 ya cement kila mmoja kama sehemu ya pongezi kwetu,”alisema Sanga.

No comments

Powered by Blogger.