Full-Width Version (true/false)


Wachezaji wa Azam FC Wampongeza John Bocco “Wewe ni Mshindi wa Kweli”

Baada ya nahodha wa Simba John Bocco kunyanyua ndoo ya VPL 2017/18 akiwa nahodha wa Simba SC nahodha wa Azam FC Himid Mao Mkami amekuwa mchezaji wa kwanza wa Azam kumpongeza Bocco.

Kabla ya kuhamia Simba, Bocco alikuwa nahodha wa Azam huku Himid akiwa nahodha msaidizi wa klabu hiyo. Kwa pamoja wawili hao msimu wa 2013/14 walishinda kwa mara ya kwanza taji la VPL katika historia yao ya ligi kuu huku ikiwa ni mara ya kwanza pia kwa klabu.Baadaye John Bocco pamoja na Aishi Manula, Shomari Kapombe na Erasto Nyoni waliondoka Azam baada ya mikataba yao kumalizika na kujiunga na Simba. Wachezaji hao wanne wakiwa katika msimu wakwanza Simba, wameshinda VPL wakiwa wachezaji muhimu kwenye kikosi cha kwanza cha Simba.

Kupitia ukurasa wa Instagram Himid ameandika:
“Hongera sana ndugu yangu John Bocco hakika wewe ni mshindi wa kweli bila maneno mengi. Ulistahili ubingwa.”

Katika post hiyo ya Himid, nahodha masidizi wa Azam kwa sasa Salum Abubakar ‘Sure Boy’ amempongeza pia Bocco kwa kuandika:
“Hongera wewe mkuu John Bocco.”

No comments

Powered by Blogger.