Full-Width Version (true/false)


Wachezaji wa Yanga waliyogoma wameenda Mbeya? Dismas katoa majibu


 

Jumanne ya May 8 2018 timu ya Yanga iliwasili Dar es Salaam ikitokea Algeria ilipokuwa inacheza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya Makundi ya Kombe la shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger, game ambayo Yanga ilipoteza kwa magoli 4-0.

Baada ya kurejea Dar es Salaam leo wachezaji wa Yanga wamesafiri kuelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons, hivyo AyoTV ikaongea na afisa habari wa Yanga Dismas Ten na kumuuliza vipi wachezaji waliyogoma kwenda Algeria wameungana na timu?

“Ni kweli timu imesafiri kuelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo wa tarehe 10 dhidi ya Prisons ni mchezo muhimu tunahitaji matokeo ili kutengeneza heshima kwenye Ligi, ndio wapo wachezaji waliyobaki nyumbani kwa matatizo mbalimbali lakini tayari wameshaungana na timu kuelekea Mbeya”>>> Dismas Ten

No comments

Powered by Blogger.