Full-Width Version (true/false)


Wachimbaji wa Madini Wanne Wafariki Dunia Baada ya Kufukiwa Mgodini

Kutoka nchini Afrika Kusini, wachimbaji wa madini wanne wanaripotiwa kufariki dunia baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi wakiwa machimboni, na kufunikwa na mgodi.

Wachimbaji hao ni miangoni mwa wachimbaji wengine 10 waliookolewa katika mgodi huo wa dhahabu ulioko Magharibi jijini Johannesburg.

Inaelezwa kuwa wachimbaji watatu bado wamenasa katika mgodi huo.

Afrika Kusini ni nchi inayoongoza kwa uzalishaji wa madini ya dhahabu lakini imekuwa ikituhumiwa kwa kuwa na rekodi ya usalama dhaifu.

No comments

Powered by Blogger.