Full-Width Version (true/false)


Wadau wakosoa sherehe ya ndoa ya Alikiba iliyofanyika Dara

 HATA ujipange vipi kuandaa sherehe ya kufa mtu, lakini ukijikwaa kidogo tu, watu wanakushukia! Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’, yamemtokea hivi karibuni baada ya kuzua mjadala akidaiwa kulikoroga kwenye sherehe ya Maulid ya harusi yake aliyofanya katika Hoteli ya Serena iliyoko jijini Dar es Salaam, kufuatia ndoa aliyofunga wiki mbili zilizopita nchini Kenya kwa kumuoa Amina Khaleef.

Kilichomponza Kiba pamoja na kufanya sherehe baa’bkubwa na ya kisasa ni kitendo chake ya kuchanganya maudhui ya kidini na kidunia katika “pishi moja” jambo linalodaiwa kuwakera wengine hasa wenye imani zao.

“Huwezi kualika Kaswida, mashehe na watu wenye imani ya dini ya Kiislamu halafu wakati huohuo ukawaita na wasanii wa muziki wa dunia nao waje waburudishe.

“Alichotakiwa kufanya ni kuchagua jambo moja, kuwaita wasanii wenzake au watu wa dini wasindikize kwenye sherehe yake,” alisema Shehe Matema, mkazi wa Kariakoo aliyehudhuria pati hiyo.

Wakati mtu huyo wa Mungu akitoa maelekezo yao ya kiimani juu ya Kiba, kwenye mitandao ya kijamii nako kulikuwa kumechafuka si kitoto, kila mtu akisema lake, huyu anasifia yule anaponda.

“Tatizo la Wabongo ni wivu, wakiona mtu kafanya kitu kizuri, basi wanatafuta kosa ili tu wapate la kusema, bora Kiba kawafunga midomo,” alisema Aneth Mosha aliyechangia kwenye moja ya mitandao wa kijamii ambao hakuna sababu ya msingi kuutanda.

Aidha, timu ya upekuzi wetu wa ubuyu mitandao ilibaini kwamba, hoja zilizobishaniwa zaidi zilikuwa ni Kiba kuchanganya mambo ya dini na kidunia katika sherehe hiyo huku suala la mavazi ya Bibi Harusi na wasanii wa kizazi kipya kupewa nafasi ya kutumbuiza likibishaniwa sana.

“Ukimwangalia Bi Harusi (Amina) alivyokuwa amevaa, huwezi kusema hayo ni maadili ya Dini ya Kiislamu, alikuwa mabega wazi, kifua wazi, hilo ni jambo baya kabisa,” alisema Shehe mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Ustadh Juma, mkazi wa Magomeni jijini Dar.

Ikumbukwe kuwa shehere hiyo ya Kiba ilimjumuisha pia mdogo wake aitwaye Abdul Kiba ambaye naye kwa upande wake alifunga ndoa na Wahid, mkazi wa Zanzibar.

Katika sherehe hiyo ya jijini Dar, viongozi mbalimbali wa kidini, kiserikali, wasanii mbalimbali wa maarufu walihudhuria huku mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk Jakaaya Mrisho Kikwete, mama Salma Kikwete akipewa nafasi ya kuwahusia wanandoa hao.

Mastaa ya mastaa waliohudhuria ni pamoja na Christian Bella, Mwana-FA, Ommy Dimpoz, Vanessa Mdee, Mimi Mars na wengine wengi.

No comments

Powered by Blogger.