Wafanyakazi wanalia, wafanyabiashara, watu wote wanalia inawezekanaje?- Mbunge ahoji

Mbunge wa Kuteuliwa(CCM), Abdallah Bulembo amesema kuwa Waziri wa
Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina hawatendei haki Watanzania hasa sekta ya
uvuvi kwa Operation ya uvuvi haramu aliyomtaka aisimamishe kwa kile
alichodai inaumiza wavuvi.
Bulembo ameyasema hayo, wakati akichangia Bajeti ya Wizara ya Mifugo
na Uvuvi ya mwaka 2018/019 ambapo amesema haiwezekani Wafanyakazi
wanalia, wafanyabiashara, watu wote wanalia inawezekanaje?
Aidha Bulembo aliongeza kuwa Kama Waziri hawasikilizi watu wa seta yake Uwaziri wake ni nini? alihoji kwa uchungu.
“Kuna wavugaji wapo hapo nje wanalalamika ngo’mbe wao wameuzwa, hii
haipo ndani ya Ilani ya CCM kwamba Waziri utakuwa baada ya kumsaidia
Rais unamsababishia matatizo, Msimchanganye Rais na Rais hawezi
kushangilia wananchi wanateswa, hawezi kushangilia wananchi wake
wanaumizwa, Rais amepigiwa kura anatakiwa kurudi kuomba kura kule
kwanini mnamchanganya Rais na matatizo ya mtu mmoja ambaye ni Waziri?,”
alihoji.
No comments