Full-Width Version (true/false)


Walimu Shule za Sekondari wapewa onyo Dar, Msingi wasifiwa

Tume ya Utumishi wa Walimu Tanzania (TSC), imewashukia walimu mkoani Dar es Salaam, hususani katika shule za sekondari kutokana na matokeo mabaya katika mitihani na kuonya kuwa walimu wazembe kamwe hawatavumiliwa.

Hayo yamesemwa leo Mei 3 na Katibu wa TSC, Winfrida Rutahindurwa, alipokuwa akizungumza na walimu wa shule za msingi na sekondari jijini Dar es Salaam.Winfridah amesema, inasikitisha shule za Dar es Salaam, kushika mkia katika matokeo ya mitihani ya taifa na kuzidiwa hata na shule za kata mikoani.

“Dar es Salaam tunatia aibu. Haiwezekani shule za sekondari kama Tambaza na Azania leo hii zinashika mkia wakati zilikuwa zinazoongoza kitaifa.Walimu mnafanya nini?,” alihoji.

Aliongeza kuwa jukumu la kwanza la mwalimu ni kufundisha lakini inavyoonekana walimu wengi Mkoani hapa hawawajibiki kikamilifu na badala yake wanafundisha watoto kwa kukariri zaidi kuliko kuelewa.

“Natoa agizo kwa walimu wakuu kusimamia taratibu na sheria za kazi.Mwlimu yeyote atakayeenda kinyume cha sheria mwajibisheni bila kujali anauhusiano gani na kiongozi yeyote serikalini,”alisema katibu huyo.
Aliongeza; “Hivi degree walizonazo walimu ni za nini?Ni kwaajili ya kuwafundisha wanafunzi au kuziweka katika kabati?Nimebaini mnafundisha wanafunzi kwa kukariri.

Acheni kutumia vitabu vyenye maswali na majibu katika kufundisha. Achaneni na vitabu vya Nyambari Nyangwine ni Bomu,”

Aidha mamlaka ya TSC inaanzia kwa mwalimu mkuu hivyo mwalimu mkuu huyo anamamlaka ya kumwajibisha mwalimu yoyote kwa mujibu wa sheria na hakuna atakaye hoji.

“Msiwaogope hao wake wa mawaziri, majaji au viongozi.Wako chini yenu. Wasiwatawale shuleni. Mbona Mke wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne (Jakaya Kikwete), Sama, alikuwa ni mwalimu na hakuwahi kujiinua?

Rais wa Awamu ya Tano (Dk. John Magufuli) mkewe ni mwalimu lakini hatukuwahi kusikia anamatatizo? Kwanini hao wengine?Wawajibisheni msiwaogoe,”

Pia katibu huyo ameonya tabia ya baadhi ya viongozi serikali, wakurugenzi, wabunge, wakuu wa mikoa na wilaya, kuingilia maamuuzi katika kuwawajibisha walimu.

No comments

Powered by Blogger.